-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

 

MATUMAINI ya kiungo mkabaji wa Simba, Gerson Fraga raia wa Brazil kurejea uwanjani kwa msimu huu yamefutika baada ya benchi la ufundi la timu yake kuweka wazi kuwa ataukosa msimu mzima kutokana na majeraha.

 

Benchi hilo linaloongozwa na Mbelgiji, Sven Vandenbroeck, limeweka wazi kuwa Fraga atakaa nje kwa zaidi ya miezi sita kutokana na majeraha ya goti aliyoyapata.

 

Kiungo huyo Mbrazili aliumia kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara wakati Simba walipokuwa wakipambana na Biashara United na kushinda 4-0 Septemba 20 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Sven ameliambia Championi Jumatatu, kuwa kwa sasa atamkosa kiungo huyo kwa mechi za msimu zilizobakia kutokana na Fraga kutakiwa kukaa nje kwa miezi sita ijayo kwa ajili ya kujiuguza majeraha yake.

 

Wakati Fraga akiukosa msimu mzima, Sven ameongeza kwamba washambuliaji wake Meddie Kagere na Chris Mugalu watarudi uwanjani baada ya wiki chache zijazo.

 

“Kagere ana majeraha ya muda mrefu lakini anaweza kurudi baada ya wiki mbili au tatu mbele kama ilivyo kwa Mugalu lakini kwa Fraga nina habari mbaya kwa sababu atakuwa nje kwa miezi sita ijayo, tutammisi Fraga hadi mwisho wa msimu,” alimaliza Sven.

MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

 

The post Fraga Majanga, Nje Msimu Mzima appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand