-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

MASTAA wa Azam FC, Mzimbabwe, Prince Dube na Obrey Chirwa wanatarajiwa kulamba tuzo ndani ya kikosi hicho baada ya uongozi wa timu hiyo kuanzisha tuzo za mwezi za timu hiyo.

 

Mastaa hao sambamba na wengine wa kikosi hicho watapambania tuzo hizo ambazo zitaanzia kwa mchezaji bora wa mwezi Septemba na Oktoba huku mashabiki wa timu hiyo wakipewa nafasi ya kupiga kura.

Msemaji wa Azam FC, Thabith Zakaria ‘Zaka Zakazi’, amesema kuwa mchakato wa kurejesha tuzo umekamilika ambapo kwa sasa wataanza kutoa kwa wachezaji waliofanya vizuri mwezi Septemba na Oktoba.

 

“Utoaji wa tuzo za ndani ya timu ulikuwepo kwa kipindi cha nyuma lakini ulipotea baada ya wadhamini ambao walikuwa sehemu ya mchakato huo kujitoa.

 

“Kwa sasa zimerudi na tunaanza kutoa tuzo hizo kwa mashabiki kupiga kura kumchagua mchezaji bora wa mwezi Septemba na Oktoba,” alimaliza Zaka.

The post Dube, Chirwa Kulamba Tuzo Azam appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand