-->

Type something and hit enter

On
 AMINI usiamini, sasa ni wazi kuwa zile kelele juu ya usajili wa kiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama, zimeisha namna hii, baada ya kuvuja kwa siri ya kwamba tayari Simba imemalizana na mchezaji huyo kwa kumpatia mkataba wa miaka miwili, kwa dau nono la dola 250,000, sawa na Sh milioni 575.

 

Tangu Jumamosi iliyopita baada ya kumalizika kwa mechi ya Yanga na Simba kwa sare ya bao 1-1, gumzo la jiji kwa sasa ni juu ya Yanga kumtangazia Chama kitita cha dola laki mbili (200,000), jambo ambalo limebadili upepo wa mchezo na kujikuta wengi wakibishana juu ya hatima wake.


Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

 

Chanzo makini kutoka ndani ya Simba, kimelinyetishia Championi Ijumaa kwamba, tayari Chama ameshavuta kitita cha dola 250,000 za Mohamed Dewji ‘MO’, ambazo zimemfanya akubali kuongeza kandarasi ya miaka miwili klabuni hapo.

 

Chanzo hicho kimeliambia gazeti hili kuwa tayari Chama ameshapewa dola 240,000 na akasaini mkataba wa awali, hivyo bado anadai dola 10,000 tu (Sh milioni 23) kabla ya kufunga ukurasa huo juu ya mkataba wake. Pamoja na dau hilo, Chama ameshakubaliana na Simba kuwa atalipwa mshahara mnono wa dola 8,500 (sawa na karibu Sh milioni 20) kila mwezi.

 

“Naomba uniamini mimi kuwa Yanga hawana uwezo tena wa kumnasa Chama, maana ishu ilimalizika tangu Novemba 5, mwaka huu, kwani siku hiyo mapema tu, CEO wetu Barbara Gonzalez, akiwa sambamba na aliyekuwa CEO wetu wa zamani, Clescentius Magori walimaza mchezo mzima.

 

“Ishu ilikuwa hivi, baada ya uongozi wetu kuona habari za kuisha mkataba wa Chama zinazidi kuwa kubwa, ulilazimika kumchukua na kukaa naye chini ambapo Chama alitaja ukweli kutakiwa na Yanga na kwamba walikuwa tayari wameshamtajia ofa ya dola 200,000, ambapo Mo, alimuongezea 50,000 na kujikuta akimshawishi kwa kumsainisha kwa dola 250,000.

 

“Hata mshahara walimalizana kwa ahadi ya kumlipa dolla 8, 500 kwa kila mwezi, jambo linaloashiria wazi kuwa Chama ataendelea kuwa mali ya Simba hadi mwaka 2023,” kilisema chanzo hicho. Championi Ijumaa lilimtafuta Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez ambaye simu yake haikupokelewa muda wote jana mchana na hata alipotafutwa Ofi sa Habari, Haji Manara naye hakupokea simu.

Click to comment
 
Blog Meets Brand