-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KIUNGO mchezeshaji wa Simba, Clatous Chama, ameibuka na kuweka wazi shauku yake ya kumuona kaka yake, Adrian Chama akijiunga naye ndani ya kikosi hicho cha Simba.

 

Chama ameongeza kuwa, anatamani ndugu yake huyo atue Simba kutokana na kuwa na uwezo mkubwa kumzidi hata yeye. Adrian anayecheza nafasi ya beki wa kati ndani ya kikosi cha Zesco United, alijiunga na kikosi hicho Julai Mosi, 2019.

 

Mzambia huyo mwenye mabao manne katika Ligi Kuu Bara, aliweka wazi suala hilo la kutamani Adrian anayeichezea Zesco United ya Zambia wakati akijibu swali aliloulizwa kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram.

 

Chama aliulizwa kuwa kama anatamani Adrian mwenye miaka 31 asajiliwe Simba na kusema ndiyo huku akiongeza kwamba Adrian ana uwezo mkubwa wa kisoka kumzidi yeye. “Ndiyo ndiyo, kwa sababu Adrian ana uwezo kuzidi mimi.”

 

Chama amekuwa akitajwa kuwa mchezaji bora zaidi wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa misimu miwili akiwa ametwaa tuzo hiyo mara mbili.

Said Ally, Dar es Salaam

 

The post  Chama Amvuta Kaka yake Simba SC appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand