-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

BIG bosi wa benchi la ufundi la Yanga, Mrundi Cedric Kaze, amefunguka kuwa licha ya mwenendo usio mzuri walionao wapinzani wao Gwambina FC lakini bado wataingia uwanjani kesho Jumanne wakiwa wanawaheshimu.

 

Kaze ameongeza kuwa kinachowafanya waingie wakiwa wanawaheshimu wapinzani wao ni kuwa wapo nyumbani kwao lakini mawazo yake ni kupata pointi tatu mbele yao.

 

Kaze kwa mara nyingine leo Jumanne ataiongoza Yanga kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara kupambana na Gwambina FC katika muendelezo wa mechi zao za Kanda ya Ziwa.

 

Mrundi huyo ameliambia Championi Jumatatu, kuwa licha ya nia yao ya kutwaa pointi tatu lakini watakuwa makini kwa sababu wapinzani wao wana safu nzuri ya ushambuliaji na pia wanacheza uwanjani kwao.

 

“Kuhusiana na Gwambina wao wako nyumbani na wamefanya vizuri kwenye eneo lao la ushambuliaji. Hatuwezi kuwadharau kwa sababu walifungwa mechi iliyopita kwa mabao 3-0 na KMC.

 

“Tunaingia kwa nguvu kubwa kwenye mechi hiyo tukiwa na nia ya kutaka kupata pointi tatu kama ambavyo tumefanya kwenye mechi zilizopita,” alimaliza Kaze.

SAID ALLY, Dar es Salaam

The post Cedric Kaze Aitangazia kiama Gwambina appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand