-->

Type something and hit enter

On
 HII ni sehemu ya mashairi yenye hisia za kutosha kutoka kwenye Ngoma ya Sumu ya Penzi ya Belle 9.Ni zaidi ya miaka 10 iliyopita tangu ngoma hii itoke, lakini bado melodi na midundo yake inasikika. Ni miongoni mwa ngoma za zamani (TBT) za Bongo Fleva zinazosikilizwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii.

Ni kutoka kwa mwanamuziki mkali wa RnB Bongo, Abednego Damian ‘Belle 9’.


Kwa kuweka kumbukumbu sawa, Belle 9 aliweza kutoka kimuziki mwaka 2009 akitokea Mji Kasoro Bahari, Morogoro pale Mtaa wa Mafinga.


Belle 9 alitoka na Sumu ya Mapenzi kisha Masogange ambazo zilimtambulisha vizuri kwenye medani ya Bongo Fleva.


Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Baada ya Sumu ya Penzi na Masogange, Belle 9 alikiwasha kinoma na ngoma nyingine kama Wewe ni Wangu, Nilipe Nisepe, Umenitupa, Ladha ya Mapenzi, House Boy, Wanitaka, Burger Movie Selfie, Umefanana Naye, Vitamin Music, Wewe Nami, Listen, Shauri Zao, Amerudi na nyingine kibao (ni zaidi ya 50).


IJUMAA SHOWBIZ imepiga stori nyingi na Belle 9 ambaye anafunguka mambo mengi kwenye exclusive interview ikiwemo ishu nzima ya kugeukia kwenye muziki wa Injili;

IJUMAA SHOWBIZ: Ni miezi imepita sasa tangu kutokea kwa ile ajali mliyokuwa na Lulu Diva na Bonge la Nyau mpaka sasa hali yako iko vipi?

BELLE 9: Kwa sasa ninaendelea vizuri, naweza kusema nimepona kabisa na ninamshukuru Mungu kwa hilo.

IJUMAA SHOWBIZ: Hongera kwa kazi nzuri unazoendelea kuzifanya kwenye muziki wako…

BELLE 9: Ahsante sana, ninashukuru.

IJUMAA SHOWBIZ: Kuna ngoma ambayo umeitoa ya Injili inakwenda kwa jina la Ahsante, labda sababu ya wewe kutoa wimbo kama huo ni nini?

BELLE 9: Kwanza kabisa ni kwa sababu ya kumshukuru Mungu kwa mengi ambayo ameweza kunitendea miujiza maana bila yeye nisingekuwa hapa nilipo.

IJUMAA SHOWBIZ:Unazungumziaje mapokezi ya ngoma hiyo?

BELLE 9: Ni mazuri sana kwa kweli mashabiki wameupokea vizuri.

IJUMAA SHOWBIZ: Labda tutegemee kuwa kwa sasa hivi Belle 9 ameamua kumtumikia Mungu au hapo hilo limekaaje?

BELLE 9: Watu wasitegemee sana, lakini mimi ni msanii, chochote kinaweza kutokea.

IJUMAA SHOWBIZ: Kwenyekutoa ngoma za Injili huwa kuna masharti ambayo lazima uyafuate, kwa upande wako umepitia ugumu gani kwenye kuandaa ngoma hiyo?

BELLE 9: Mimi nashukuru sana kwa kuwa sikuweza kupata changamoto yoyote, hata ukifuatilia ni wimbo ambao sijautunga ila nimeongelea vitu ambavyo vipo kwenye maisha yetu.

IJUMAA SHOWBIZ: Tangu enzi za Ngoma za Masogange, Sumu ya Penzi, Wewe ni Wangu na nyingine, nini siri ya kudumu kwa ngoma hizo?

BELLE 9: Kwanza ni mapenzi ya kazi maana napenda sana ninachokifanya, mara nyingi huwa nasema napenda kile ninachokifanya.

IJUMAA SHOWBIZ: Kwawasanii wasiodumu, je, unadhani wanakwama wapi?

BELLE 9: Si kwamba ni kitu kinachowakwamisha, inaweza ikawa si wito wa mtu ila kwa sisi tunaoendelea ni kukomaa na kubaki kwenye mstari.

IJUMAA SHOWBIZ: Mipango ya kuachia album kwa upande wako imekaaje?

BELLE 9: Kwa sasa hivi bado, labda hadi mwakani.

IJUMAA SHOWBIZ: Mbali na kazi zako mwenyewe pia ulionekana kufanya kolabo na wasanii tofautitofauti, mipango iko vipi ya kufanya kazi nyingine?

BELLE 9: Mipango ipo ya kufanya kazi nyingine, mashabiki wakae tu tayari.

IJUMAA SHOWBIZ: Upepo wa muziki uko vipi ukilinganisha na zamani?

BELLE 9: Muziki haujawahi kuwa rahisi hata siku moja, gemu ni gumu sana na biashara ya muziki imekuwa na njia nyingi za kuukuza.

IJUMAA SHOWBIZ: Ni muda sasa tangu umeoa, lakini umekuwa ni mtu wa kuficha uhusiano wako, sababu ni nini hasa?

BELLE 9: Hakuna sababu yoyote, lakini mimi sioni haja ya kuweka mambo yangu mengine hadharani, nadhani mashabiki wamenijua mimi kwenye muziki, wanatakiwa wanijue hivyohivyo.

IJUMAA SHOWBIZ: Nini siri ya kudumu kwenye ndoa yako?

BELLE 9: Ni kumuomba Mungu na kuwa rahisi kuomba msamaha na kusamehe.

IJUMAA SHOWBIZ: Ni kweli ndoa zinayumbisha muziki?

BELLE 9: Katika fani yoyote ni lazima uzingatie familia yako kwanza, hata kwa upande wangu ninaitanguliza sana familia.

IJUMAA SHOWBIZ: Mkeo ana sapoti gani kwenye kazi zako?

BELLE 9: Anakubali kazi zangu maana amekubali kuwa na mwanamuziki.

IJUMAA SHOWBIZ:Nikupongeze kwa kutokuwa na skendo kwenye fani yako, je, ni kitu gani kimesimama nyuma yako?

BELLE 9: Kiukweli ukimuachia Mungu maisha yako, hakuna jambo baya ambalo litakusumbua.

IJUMAA SHOWBIZ: Umejipanga vipi kwenye kufikisha muziki wako kimataifa zaidi?

BELLE 9: Kwangu umeshafika tayari.

IJUMAA SHOWBIZ: Mashabiki wangependa kufahamu Belle 9 ni mtu wa aina gani?

BELLE 9: Ni mtu mzuri sana, ana heshima, mcha-Mungu na pia ni mtu ambaye nipo na maisha yangu, ninapambana.

Click to comment
 
Blog Meets Brand