-->

Type something and hit enter

On
 BAO la kusawazisha la beki wa kati, raia wa Kenya, Joash Onyango, limezuia Sh milioni 500 walizoahidiwa wachezaji wa Yanga kama wangewafunga watani wao wa jadi, Simba.

Mkenya huyo ambaye kabla ya kufunga bao hilo la kusawazisha kwa njia ya kichwa, akitumia mpira wa kona uliopigwa na Luis Miquissone, alisabisha penalty dhidi ya timu yake, baada ya kumchezea vibaya kiungo Mkongomani Tuisila Kisinda na Mghana Michael Sarpong akafunga.


Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara, hatimaye ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 juzi.


Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatatu, awali kamati mpya ya Mipango na Ushindi ya Yanga ilitoa ahadi ya Sh milioni 150 kabla ya siku ya mchezo huo wadhamini wa timu hiyo, Kampuni ya GSM kuongeza Sh milioni 350 na kufikia mil 500.


Mtoa taarifa wetu alisema kuwa mabosi hao walitoa ahadi hiyo ya

fedha katika kikao cha pamoja kati ya viongozi, wachezaji na benchi la ufundi kilichofanyika kwenye kambi yao Kijiji cha Avic Town, Kigamboni jijini Dar es Salaam.


Aliongeza kuwa kikao hicho kilikwenda sambamba na chakula cha jioni na baada ya hapo mabosi hao wakatoa ahadi hizo za fedha ikiwa siku moja kabla ya mchezo na lengo likiwa ni kuwaongezea morali ya ushindi ili vijana wao wapambane.


“Sare hii tuliyoipata ya bao 1-1 imewaumiza wachezaji wetu sana, hiyo ni kutokana na ahadi kubwa ya fedha waliyoahidiwa na mabosi walipokuja kutembea kambini tukiwa katika maandalizi ya mwisho ya mchezo huo dhidi ya Simba.


“Ndiyo sababu ya kuwaona wachezaji kuishiwa nguvu na kulala uwanjani mara baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa.

“Mabosi hao walitoa ahadi ya fedha ya Sh mil 500 ambayo wangepewa kama wangewafunga Simba, hivyo kama matokeo yangemalizika kwa ushindi wa bao 1-0, basi wachezaji wangeingiziwa fedha kwenye akaunti zao kesho (leo) Jumatatu.


“Lakini mabosi hao wanaangalia jinsi ya kuwapatia fedha kidogo kama bonasi baada ya kupata sare hiyo, licha ya kutokuwa malengo yao katika mchezo huo,” alisema mtoa taarifa huyo.


Matokeo hayo, yanaifanya Yanga iwe na pointi 24 katika nafasi ya pili, nyuma ya Azam kwa tofauti ya pointi moja katika mbio za ubingwa. Simba ipo nafasi ya tatu (pointi 20). Timu zote zimecheza michezo 10.


Alipotafutwa mwenyekiti wa timu hiyo, Dk Mshindo Msolla kuzungumzia hilo, simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa hadi Championi Jumatatu linatimba mtamboni.


Alipotafutwa Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela kuzungumzia hilo, alisema: “Hilo suala la ahadi ni siri kati ya viongozi na wachezaji, hivyo si vizuri kuliweka kwa uwazi.”

Mara baada ya kufunga bao hilo, Onyango alisema: “Waache waendelee kuniita mimi mzee lakini nitathibitisha uwezo wangu uwanjani kwa kufanya kazi yangu kuokoa hatari golini na kufunga mabao kila ninapopata nafasi ya kufunga kama niliyoipata leo nilipowafunga hao Yanga.”

Click to comment
 
Blog Meets Brand