-->

Type something and hit enter

On
Vatican imesema kuwa inachunguza tukio la akaunti rasmi ya Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani (Papa) ku-like picha ya mrembo aliyevaa nguo zisizo za staha.

Idara maalum katika Ofisi ya Papa inayoshughulika na vyombo vya habari imeiambia BBC kuwa wanachofahamu ‘like’ hiyo haikufanywa kwa namna yoyote na Ofisi ya Papa.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uongozi wa Vatican unafanya kazi na #Instagram kuona hiyo like ilitokea wapi.

Vyanzo kutoka Vatican vililiambia gazeti moja la Kikatoliki kuwa akaunti hiyo inasimamiwa na timu ya watu walioajiriwa na kwamba uchunguzi wa ndani pia unaendelea kubaini kama kuna mmoja kati ya watu wa timu hiyo alihusika.

Katika hatua nyingine, #Garibotto, ambaye ndiye mwanamitindo aliyepata LIKE hiyo kutoka kwenye akaunti ya Papa, yeye alisema kuwa alifurahi kuona ‘like’ hiyo na anajiona amefika Peponi.

#SNSNews


Click to comment
 
Blog Meets Brand