ARSENAL YACHANA MKEKA, YAPIGWA NA ASTON VILLA - EDUSPORTSTZ

Latest


 

ARSENAL YACHANA MKEKA, YAPIGWA NA ASTON VILLA


 EMILIANO Martinez kipa namba moja wa Aston Villa  jana Novemba 8 aliibuka shujaa baada ya kutoka na clean sheet kwenye ushindi wa mabao 3-0  dhidi ya Arsenal,  Uwanja wa Emirates. 


Mabao ya Aston Villa ambayo Mtanzania, Mbwana Samatta alicheza hapo msimu uliopita kabla ya kutolewa kwa mkopo nchini Uturuki yalifungwa na Bukayo Saka aliyejifunga dakika ya 25 na Olle Watkins alifunga mabao mawili dakika ya 72 na 75.


Ushindi huo unaifanya Aston Villa iliyocheza mechi 7 kuwa nafasi ya 6 ikiwa na pointi 15 huku Arsenal iliyocheza mechi 8 ikiwa nafasi ya 11 na pointi 12.


Vinara ni Leicester City wakiwa na pointi 18 baada ya kucheza mechi 8 na mabingwa watetezi Liverpool nafasi ya 3 na pointi 17 zote zimecheza mechi 8.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz