-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

WATANI wa Jadi Yanga na Simba jana walimenyana vikali kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa jana Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar.

Kama kawaida ilivyodabi ya watani hao wa jadi ilikuwa upinzani mkali ulioanzia na mabishano ya mashabiki na kuendelea kwa wachezaji uwanjani.

Katika kipute hicho Yanga ndiyo walioanza kupata bao la penalti dakika ya 28 Tuisila Kisinda alipofanyiwa madhambi na beki wa Simba Joash Onyango.

Penalti hiyo ilipigwa na Michael Sarpong na kuingia wavuni.

Mambo yakizidi kutifuka uwanjani hapo Onyango ni kama alikuwa akitaka kufuta lawama ambaye ingemkabili kwa kusababisha penalti na kufunga bao la kichwa mpira uliopigwa na Luis Miquissone.

John Bocco (katikati) akipambana na wachezaji wa Yanga, Feitoto kushoto na Bakari Mwamnyeto (kulia).

Farid Mussa wa Yanga (kushoto) akipiga mahesabu ya kumtoka Muzamiri Yasin.

Mashabiki wa Yanga a.k.a Wananchi wakiwa katika bonge la shangwe wakati kipute kikiendelea.

Mashabiki wa Simba a.k.a Mnyama nao walikuwa full mzuka.

Kikosi cha Yanga kilichoanza.

Kiki cha Simba kilichoanza.                                                                                                                                      HABARI NA PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL

The post Angalia Yanga na Simba Walivyomenyana Kiume Benjamini Mkapa appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand