-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

                                                  Leopoldo Luque, daktari aliyefanya upasuaji wa Diego Maradona.

WAENDESHA mashitaka nchini Argentina wanamchunguza daktari wa  Diego Maradona, Leopoldo Luque, wakimshuku kwa kuua kufuatia kifo cha nyota huyo wa soka kilichotokea Novemba 25 mwaka huu.

 

Polisi mjini Buenos Aires wameisaka nyumba na kliniki ya daktari huyo huku wakijaribu kubaini iwapo ulikuwepo uzembe katika matibabu baada ya upasuaji aliofanyiwa Maradona.

Maradona ambaye alikuwa na umri wa miaka 60 alifariki dunia kutoka na shinikizo la damu nyumbani kwake ambako alikuwa akiendelea kupona baada ya kufanyiwa upasuaji.

 

Polisi wanashuku kwamba nyota huyo wa soka aliruhusiwa  kwenda nyumbani  kwake akiwa bado hajatimiza  masharti ya  kumruhusu atoke hospitalini, ikiwemo kupewa wauguzi au nesi wa kumhudumia saa 24, wataalamu wa uraibu, kupewa daktari anayeweza kumuita wakati wowote na gari la kubebea wagonjwa lenye vifaa vya kumsaidia kupumua.

 

Maafisa wanataka kufahamu kuhusu uhusika wa daktari Luque katika mipango ya kupona kwa Maradona katika nyumba ya nyota huyo.

 

Maradona alifanyiwa upasuaji kwenye mshipa wa ubongo kutokana na kuganda kwa damu ambapo mapema mwezi wa Novemba alikuwa akipata matibabu kutokana na uraibu wa pombe.

 

Familia ya Maradona  inafuatilia kwa makini sakata hilo ili kubaini kama  dakatari huyo alifanya uzembe wakati wa upasuaji.

The post Aliyekuwa Daktari wa Maradona Achunguzwa appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand