-->

Type something and hit enter

On
 MBELGIJI Sven Vandenbroeck, amefunguka kuwa amekoshwa na viungo wake wawili Ibrahim Ajibu na Said Ndemla ambao walifunga mabao kwenye mechi yao dhidi ya Mwadui FC kwa kubainisha wazi hiyo inaonyesha hamtegemei mtu mmoja kwenye suala la kufunga.

 

Mbelgiji huyo ameongeza kuwa mabao ya viungo hao yanamfanya sasa kuona timu yake ina uwezo wa kupata pointi kwa kufunga bila ya kuwategemea washambuliaji wao ambao walikosekana kwenye mechi kadhaa nyuma kutokana na majeraha.

 

Ajibu na Ndemla walifunga mabao wakati Simba ikishinda mechi yake ya ligi kuu mbele ya Mwadui FC kwa mabao 5-0 katika Uwanja wa Uhuru, Dar juzi Jumamosi. Mabao mengine ya Simba yalifungwa na John Bocco aliyefunga mawili na Hassan Dilunga.

 

Sven amesema kuwa kitendo cha wachezaji hao kufunga kinampa wigo wa kuona wana uwezo wa kupata mabao na pointi kwenye mechi yoyote bila ya kuwategemea washambuliaji wake halisi ambao kwa sasa ni wagonjwa.

 

“Kila mmoja anaweza kufunga mabao hapa wala siyo kuwategemea Bocco, Kagere au Mugalu pekee. Ndemla, Dilunga wamefunga, ni jambo zuri na hii inafanya tuwe na mifumo mingi ya kucheza na tukapata mabao.

 

“Kocha anaweza kumpenda mshambuliaji anayefunga mabao 15 kwa msimu lakini siku ambayo akikamatwa na wapinzani timu haitafunga, hivyo kwa namna hii ya kila mtu kufunga inanifanya niwe na mbinu mbadala za kupata pointi,” alimaliza Mbelgiji huyo.

Click to comment
 
Blog Meets Brand