-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

ABDI Banda, nyota wa zamani wa Klabu ya Simba ambaye alisajiliwa na kikosi hicho msimu wa 2014 akitokea Coastal Union ya Tanga, amesema kuwa yupo tayari kusaini Simba ikiwa atapewa ofa nzuri kwa kuwa ni timu ambayo inafanikisha malengo ya wachezaji wengi.

 

Banda alisepa Bongo msimu wa 2017 na kujiunga na Klabu ya Baroka FC ya Afrika Kusini aliyodumu huko mpaka msimu wa 2019 na rekodi zinaonyesha kuwa alicheza jumla ya mechi 41 na alifunga mabao manne.

 

Beki huyo mzawa alisajiliwa na Klabu ya Highlands Park ya Afrika Kusini ambayo kwa sasa imeuzwa na kumfanya aache majukumu ya kurudi kwenye timu hiyo mikononi mwa wakala wake na kwa sasa yupo zake Bongo.

 

Banda amesema: “Ikiwa itatokea nikahitaji timu ya kusaini kwa Bongo, kipaumbele changu cha kwanza ni Simba, ukizingatia kwamba ni timu ambayo imenitoa na kunifanya nifi kie hapa nilipo, ninajua kwamba wengi wanapenda kusaini Simba.

 

“Ikiwa nitapata ofa nyingi, kipaumbele changu nitaanza na Simba lakini kitu cha msingi ni maslahi, Simba ni daraja ambalo linawapitisha wengi hata wakiondoka huwa wanakumbuka yale ambayo wamepitia.”

 

Kabla ya beki huyo kusema hayo, hivi karibuni ilielezwa kuwa Simba wanataka kuanza mazungumzo nayo na ikiwezekana wampe mkataba wa miaka miwili.

Lunyamadzo Mlyuka, Dar es Salaam

The post Abdi Banda Ajisogeza Simba appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand