-->

Type something and hit enter

OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL Ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako nakutasoma habari zote hata kama hauna MB
VIGOGO wa Misri, Zamalek wamebisha hodi Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Raja Club Athletic waliotawazwa kuwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola Pro hivi karibuni.
Na aliyewazimisha Raja ni Mmorocco mwenzao, Achraf Bencharki aliyerejea Uwanja wa Mohamed V Jijini Casablanca na kufunga bao pekee katika mchezo huo wa Nusu Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa usiku wa kuamkia leo.
Mchezaji huyo wa zamani wa Wydad Club Athletic alifunga bao hilo pekee dakika ya 18 akimalizia pasi ya Ahmed Sayed 'Zizo' na sasa The White Knights watahitaji kwenda kuulinda ushindi huo mwembamba kwenye mchezo wa marudiano Uwanja wa Kimataifa wa Cairo Jumamosi ijayo ili waende fainali.

Huo unakuwa ushindi wa pili wa Zamalek dhidi ya Raja kwenye mechi tatu za michuano ya klabu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Kwa Raja, hicho ni kipigo cha pili tu katika mechi 23 za Ligi ya Mabingwa Afrika walizocheza nyumbani, wakati Zamalek waliingia kwenye mchezo huo wakiwa na rekodi ya kushinda mechi moja tu ugenini katika mechi 13.
Ushindi wa Zamalek umeendeleza wikiendi nzuri kwa timu za Misri Jijini Casablanca baada ya Al Ahly nayo kuifunga Wydad 2-0 katika Nusu Fainali nyingine ya kwanza Jumamosi na sasa mahasimu hao wa Jiji la Cairo wanaweza kukutana wenyewe kwenye fainali kama watazitoa timu za Morocco.


Click to comment
 
Blog Meets Brand