-->

Type something and hit enter

On
 INJINIA Hersi Said, Mjumbe wa Kamati ya Usajili ndani ya Klabu ya Yanga na Mkurugenzi wa Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa klabu hiyo amesema kuwa benchi la ufundi linabaki chini ya Juma Mwambusi ambaye alikuwa ni kocha msaidizi wa klabu hiyo.


Mwambusi alikuwa akifanya kazi chini ya Kocha Mkuu, Zlatko Krimpotic ambaye alifungashiwa virago vyake ndani ya Yanga Oktoba 3 muda mfupi baada ya kutoka kukiongoza kikosi chake kushinda mabao 3-0 mbele ya Coastal Union.


Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Hersi amesema:"Kwenye benchi la ufundi ameondolewa Zlatko peke yake, hivyo kwa sasa timu itakuwa chini ya Juma Mwambusi pamoja na wale wengine aliokuwa akifanya nao kazi.

"Kikubwa kwa sasa tunaangalia namna gani tunaweza kumpata mrithi wake ila hakuna kitakachoharibika kwani mipango inakwenda vizuri mashabiki na wadau wasiwe na mashaka taarifa watazipata muda sio mrefu."

Zlatko amekiongoza kikosi kwenye mechi tano za ligi ambapo alilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons na alishinda mechi nne akifikisha jumla ya pointi 13 kibindoni.

Kwenye mechi zake zote ambazo alikuwa benchi timu yake haikupoteza mchezo.

Click to comment
 
Blog Meets Brand