YANGA YADAI MKATABA WA MORRISON SIMBA SIO HALALI - EDUSPORTSTZ

Latest


 

YANGA YADAI MKATABA WA MORRISON SIMBA SIO HALALI


 KLABU ya Yanga imeibua upya utata mwingine wa mkataba wa mshambuliaji Bernard Morrison wakidai hana mkataba halali na mabosi wake wa sasa ambao ni Simba.

 Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela amesema hayo Jana Oktoba Mosi kwa kueleza kuwa wakati klabu yao ikipokonywa haki ya umiliki wa Morrison wamebaini mapungufu makubwa katika mkataba wa mchezaji huyo na Simba.


 Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Mwakalebela ambaye amekuja na nakala anayodai ni ya mkataba huo amesema sehemu zote za mkataba huo zimesainiwa na mchezaji huyo pekee hatua ambayo sio sahihi.

 

Amesema katika mkataba huo pia hauna sehemu iliyosainiwa na kiongozi yoyote wa bodi ya Simba lakini pia hauna saini ya shahidi.

 

Pia,amesema katika kila nakala imesainiwa na Morrison pekee bila ya upande wa pili hatua ambayo inaoonyesha watani wao hao hawakuridhia mkataba huo.

 

“Una mapungufu makubwa katika sehemu mbili…hakuwa na shahidi lakini amesaini kwenye upande wake, CEO wa Simba hajasaini. Simba SC haijaridhia mkataba wa Morrison kwa sababu hakuna sehemu yoyote ambapo klabu ya Simba imesaini mkataba wa Morrison.

 

"FIFA inamtambua Morrison ni mchezaji wa Yanga. TMS ya FIFA inamtambua Morrison mchezaji wa Yanga. Mkabata wa Simba na Morrison una dosari, upande wa mchezaji umesainiwa bila shahidi,”  amesema Makamu Mwenyekiti Yanga, Fredrick Mwakalebela.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz