-->

Type something and hit enter

On
 KIUNGO wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amesema kuwa anaamini mbele ya kocha mpya wa timu hiyo, Cedric Kaze, kikosi chao kitafanya vizuri msimu huu kwa kupata ushindi katika michezo ya ligi kuu na michuano mingine.

 

Oktoba 15 Kaze alisaini mkataba wa miaka miwili kuinoa Yanga na Oktoba 16, jana Jumamosi alianza kazi rasmi ya kuwanoa wachezaji wake wanaojiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 22, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.


Kocha huyo amekuja kuchukua mikoba ya Mserbia, Zlatko Krmpotic ambaye alitimuliwa usiku wa Oktoba 3, mwaka huu, muda mchache baada ya kuiongoza Yanga kuifunga Coastal Union.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Fei Toto alisema anaamini kupitia kocha huyo, timu yao itaendelea kupata ushindi katika michezo ijayo ya ligi kwani mipango mikubwa iliyopo ni kuhakikisha kushinda kila mechi.

 

“Mipango ya timu ni kuhakikisha tunashinda katika kila mchezo ambao upo mbele yetu, hakuna mchezaji wala kiongozi ambaye anapenda kuona timu ikifungwa, hata kwa upande wa kocha mpya itakuwa ni hivyo.

 

“Ingawa hatujakaa naye sana, lakini tunaamini anahitaji kuona timu ikizidi kupata mafanikio, kwa upande wangu namkaribisha, naamini atatupa mbinu nzuri za ushindi,” alisema kiungo huyo.

Click to comment
 
Blog Meets Brand