-->

Type something and hit enter

On
 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mechi za ligi pamoja na nyingine zote bila kujali inakutana na nani ndani ya uwanja.


Jana, Yanga ilishinda bao 1-0 mbele ya Mwadui FC kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.


Bao pekee la ushindi lilifungwa na Michael Sarpong dakika ya 81 na kuwafanya mashabiki wa Yanga kusepa na furaha kwa ushindi kwenye mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkubwa.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya ushindani na wanatambua kwamba kila mechi ni ngumu na wapinzani wao wanakuwa wakiwakamia kupata ushindi.

"Kila mchezo kwetu ni mgumu kwa kuwa wapinzani wetu wanapambana ndani ya uwanja, kila timu ambayo inakuja uwanjani inatambua kwamba inakuja kupambana na timu kubwa.

"Kikubwa mashabiki wetu sapoti katika hili kwani kila mchezaji anatambua kwamba kwa sasa tunahitaji kushinda mechi zetu hivyo kikubwa tutazidi kupambana, tupo tayari," amesema.

Yanga ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 13 imecheza mechi tano imefunga mabao saba na kufungwa bao moja.  

Click to comment
 
Blog Meets Brand