-->

Type something and hit enter

On
 Anaandika Saleh Jembe kwenda kwa Haji Manara namna hii:-

HAJI Manara umekuwa kivutio kwa vijana wengi kutamani kuwa wasemaji wa klabu, kazi ambayo miaka minne tu nyuma, hakuna aliyetamani kuifanya.


Ubunifu wako, uthubutu bila ya woga umefanya uibadilishe nafasi hiyo kutoka kuonekana ni ya watu wazima tu na sasa vijana wanaona ni kazi ya heshima na ufahari kuifanya.

Wasemaji wengi wametamani kufikia ulipo au kukupita na hii ni NEMBO YA MAFANIKIO.

Hakuna msemaji hata mmoja Afrika hii ameweza kutengeneza au kuichagiza misemo kadha wa kadha na sasa imekuwa misemo ya mpira ambayo imekuwa burudani, furaha na faraja ya mashabiki wa klabu yako ya Simba.

Umeanzisha kampeni kadha wa kadha, ukiwachambua na kuwadadavua wachezaji wa Simba na uwezo walionao kuwapa nguvu ya ushawishi Wanasimba wafike pale kwa MKAPA.

Nimeona NIKUSHAURI kwamba wakati mwingine kupuuzia KUNAEPUSHA mengi sana. Huwezi kujibu kila kitu na bahati mbaya sana, kila UNAPOFANYA MAZURI na kutengeneza UKUBWA, chuki huongezeka.

Kwa Tanzania, ukitaka upendwe sana ni kujipa stress. Ushauri wangu kwako, NYAMAZA TENA NYAMAZA SANA.

Najua wewe ni MZARAMO na mtani wangu, ulimi saa zote mdomo UNAWASHA...Lakini kunywa maji na UNYAMAZE.

Click to comment
 
Blog Meets Brand