-->

Type something and hit enter

On
 SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa makosa ambayo wameyafanya kwenye mechi mbili zilizopita watayafanyia kazi kwenye mechi zao zijazo ili kuweza kupata matokeo chanya.


Kocha huyo ana mtihani mgumu mwingine mbele yake wa kusaka pointi tatu mbele ya Mwadui FC ambao msimu uliopita kwenye mchezo wa ligi walipokutana mara ya kwanza Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Simba imekwama kupata pointi sita kwa kupokea vichapo viwili mfululizo ambapo ilianza kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Nelson Mandela na ilichapwa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting Uwaja wa Uhuru.

Kwenye mechi zote hizo mbili, Simba ilikwama kushinda na ilikosa penalti kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting uliochezwa Uwanja wa Uhuru baada ya nahodha John Bocco kugongesha mwamba penalti hiyo.

Sven ambaye amesema kuwa mpaka sasa hajui sababu ya vichapo hivyo anaamini kwamba watafanya vizuri mechi zijazo.

"Sikumbuki mara ya mwisho kupoteza mechi mbili nikiwa Kocha Mkuu ilikuwa lini ila mpaka sasa ninaona kwamba haya kwangu ni maajabu kutokea.

"Kwa kuwa mchezo wa mpira ni makosa, basi kwa yaliyotokea tunayafanyia kazi na kuona kwamba tutarekebisha kwenye mechi zetu zijazo," amesema.

Mchezo ujao wa Simba ni dhidi ya Mwadui FC utachezwa Oktoba 31, Uwanja wa Uhuru.

Simba ikiwa imetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 inakutana na Mwadui FC ambayo imetoka kupoteza kwa kufungwa mabao 6-1 dhidi ya JKT Tanzania.

Click to comment
 
Blog Meets Brand