-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KIWA Simba ipo nafasi ya pili baada ya kucheza mechi tano na kujikusanyia pointi 13 ndani ya Ligi Kuu Bara msimu huu, kocha mkuu wa kikosi hicho, Sven Vandenbroeck, amesema sababu kubwa inayompa nafasi Aishi Manula kukaa golini ni uwezo wake.

 

Manula amekaa golini kwenye mechi zote tano ambazo Simba imecheza mpaka sasa kwenye ligi, huku kipa namba mbili wa kikosi hicho, Beno Kakolanya akiendelea kusugua benchi bila ya kupata nafasi hata ya kudaka kwa dakika moja.

Kwenye mechi hizo tano, Manula ameruhusu mabao mawili na kuondoka na clean sheet tatu mbele ya Biashara United, Gwambina na JKT Tanzania.

 

Aliruhusu mabao dhidi ya Ihefu na Mtibwa. Sven amesema: “Kufanya vizuri kwa Manula ni sababu ya yeye kuendelea kukaa langoni, lakini haina maana kwamba wengine hawawezi kufanya vizuri, ni suala la kusubiri wakati kuona kwao itakuwaje.”

STORI: LUNYAMADZO MLYUKA, Dar

The post Sven Ataja Sababu za Kakolanya Kukaa Benchi appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand