-->

Type something and hit enter

On
 KIUNGO mchezeshaji wa Simba, Mzambia, Clatous Chama, ameweka wazi kwamba licha ya kukosa kucheza na Yanga Oktoba 18, mwaka huu lakini anaamini watazipata pointi zao kutokana na kuongezewa muda zaidi wa kujiandaa.

 Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Kiungo huyo ameongeza kwamba walikuwa wameshaanza kuitolea macho mechi hiyo ya dabi lakini kwa sasa wanaangalia mechi zijazo baada ya kupelekwa mbele.


 

Simba walipangiwa kucheza na Yanga kwenye Kariakoo Dabi Oktoba 18 lakini mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara imesogezwa mbele hadi Novemba 7.


Kiungo huyo raia wa Zambia amesema kwamba kwa sasa hawana cha kupoteza baada ya kushindwa kucheza na Yanga na wanaangalia mbele katika mechi zao zijazo za ligi.

 

“Simba kila siku iko tayari kwa ajili ya kupambana na timu yoyote ile kwa sababu msimu unaenda mbele.

 

"Mechi na Yanga ni mechi kubwa ambayo tulikuwa tunaiangalia lakini nafikiri sababu za kughairisha mechi zilizotolewa ziko vizuri.

 

“Tuna mechi nyingine hapa kati kama ratiba yetu inavyoonyesha na pale ambapo itakuja tutacheza. Nafikiri imetupa muda zaidi wa kujiandaa, hiyo ni mechi kubwa lakini naamini tutafanya vizuri,” alimaliza Chama.

Click to comment
 
Blog Meets Brand