-->

Type something and hit enter

On
 UONGOZI wa Simba umesema kuwa uwezo wa kiungo mkabaji Said Ndemla ndani ya Simba kwa msimu wa 2020/21 ni moja ya sababu ya yeye kuitwa kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania,  Taifa Stars.


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa timu ya Taifa ya Tanzania haitazamani rekodi za miaka nane ama sita ila wanatazama kile ambacho amekifanya kwa muda akiwa ndani ya Uwanja kwa wakati huo.


Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Ndemla ni miongoni mwa nyota ambao wametajwa kwenye kikosi cha  Stars kitakachoingia kambini Oktoba 5 kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Burundi unaotarajiwa kupigwa Oktoba 11, Uwanja wa Mkapa. 


Manara amesema:"Kwa namna ambavyo Ndemla anafanya juhudi na uwezo alionao anastahili kuitwa kikosi cha Stras, ni mtu anayepata namba kikosi cha kwanza na anapambana kufanya kazi makini sasa kwa nini asiitwe kwenye kikosi? 


"Kupata namba ndani ya kikosi cha Kwanza Simba sio kitu chepesi kwa kuwa kikosi ni kigumu na kina kila aina ya wachezaji wazuri, Ndemla atafanya makubwa kwa kuwa anapata namba ndani ya Simba," amesema.

Click to comment
 
Blog Meets Brand