-->

Type something and hit enter

On
 KIKOSI cha Simba leo Oktoba 19 kimeanza safari kuelekea Mbeya ambapo kitakaa kwa muda wa siku mbili kabla ya kuelekea Rukwa kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons. 

Mchezo huo wa raundi ya sita utachezwa Oktoba 22, Uwanja wa Nelson Mandela,  saa 10:00.

Leo wapinzani wao Tanzania Prisons watakuwa kibaruani Uwanja wa Jamhuri Dodoma kumenyana na JKT Tanzania mchezo wa Ligi Kuu Bara wakimaliza mchezo huo watarejea Rukwa kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Simba.


Kwa sasa Simba ni mabingwa watetezi wakiwa nafasi ya pili na pointi zao ni 13 baada ya kucheza mechi tano na safu yao ya ushambuliaji imefunga mabao 14.


Prisons ipo nafasi ya 12 ikiwa na pointi tano baada ya kucheza mechi tano na safu yao ya ushambuliaji imefunga mabao matatu.

Click to comment
 
Blog Meets Brand