-->

Type something and hit enter

On
 MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe ameibuka na kusema kuwa kitendo cha uongozi wa Yanga kumsajili mshambuliaji, Saidi Ntibazonkiza wamefanya jambo sahihi.

 

Yanga Oktoba 12 ilitangaza kumsajili mchezaji huyo kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu akiwa huru baada ya Oktoba 11,2020 kufunga bao pekee katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Taifa Stars akiwa na timu ya Taifa ya Burundi katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.


 Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


 Tambwe amesema kuwa, wapinzani wa Yanga watakuwa na kazi kubwa ya kupambana naye kwa kuwa anamjua vizuri ubora wake huku akisisitiza Yanga ilikosa mshambuliaji anayeweza kucheza namba kumi.

 

“Nimeona kwenye mitandao wanaandika lakini najua atawasaidia ila sijajua ni kocha mwenyewe ndiyo amependekeza au hiyo ni siri yao. Kuhusu mchezaji ni mzuri, anaweza kucheza kama winga wakati mwingine mshambuliaji wa kati.

 

“Najua atawasaidia kwa sababu ukiangalia wasifu wake amecheza katika ligi kubwa hivyo ana uzoefu wa kutosha, ukiona mtu anafika huko ujue anajua na kujua anajua kweli kwa sababu tulikuwa tunafanya naye mazoezi hapa Vital’O na siku nyingi tunajuana, nafikiri wapinzani wa Yanga haswa Simba watapata shida sana,” amesema Tambwe.

Click to comment
 
Blog Meets Brand