-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

BAADA ya kuchezea vichapo viwili mfululizo timu ya Simba leo, Jumamosi, Oktoba 31, 2020, imeshinda kwa kishindo baada ya kuichapa Mwadui Fc mabao 5-0, mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao umepigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

 

Kurejea kwa fundi Clautous Chama na nahodha John Bocco kumeonekana kuwapa uhai Simba na kufanikiwa kupata magoli kupitia kwa Bocco aliyefunga magoli mawili kwenye dakika ya 25 na 64 na Ibrahim Ajibu akitokea benchi akafunga bao dakika ya 81.

 

Sub za kocha Sven zilionekana kuwa na faida baada ya Hassan Dilunga kufunga kwenye dakika ya 87 na Said Ndemla kuhitimisha karamu hiyo dakika za lala salama, Mwadui baada ya mechi tisa wamefikisha pointi tisa wakiwa katika nafasi ya 15.

 

Simba imefikisha pointi 16 kwenye msimamo wa ligi wakiwa nafasi ya tatu mechi inayofuta ni dhidi ya watani wao wa jadi Yanga.

The post Simba Sc Yaipa Kipigo Hevi Mwadui appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand