-->

Type something and hit enter

On
 KIKOSI cha Simba chenye mastaa wenye ushkaji na nyavu ikiwa ni pamoja na Chris Mugalu, Meddie Kagere, Clatous Chama kina kazi ya kuyeyusha dakika 180 ambazo ni mechi mbili za kirafiki Oktoba 13 na 17.

Mugalu ana mabao matatu, Kagere mabao manne na Chama yeye amefunga mabao mawili na pasi mbili za mabao.

Mechi zote mbili ambazo ni maalumu kwa ajili ya kujiweka fiti kwa ajili ya mechi za ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara ikiwa ni pamoja na ile dhidi ya Yanga itakaypopigwa Novemba 7 badala ya Oktoba 18.

Oktoba 13, Simba itacheza na Ndanda FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza na Oktoba 17 itacheza na Mlandege FC ya Zanzibar.


 Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa mechi hizo ni maalumu kwa ajili ya kujweka sawa na wanaamini itakuwa ni kipimo tosha kwao kufanya vizuri kwenye mechi zao zijazo.


"Kuhusu mchezo wetu dhidi ya Yanga huo sisi hatuna cha kusema kwa kuwa kazi yetu sisi ni kucheza na sio kupanga ratiba, tuna mechi za kirafiki ambazo lengo lake ni kutufanya tuzidi kubwa imara, mashabiki wajitokeze kwa wingi," amesema.


Mechi zote mbili Simba itacheza Uwanja wa Azam Complex na itakuwa kuanzia saa 11:00 jioni. 

Click to comment
 
Blog Meets Brand