-->

Type something and hit enter

On
 


Nyota wa timu ya Taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo amekutwa na maambukizi ya virusi vya Corona na ataukosa mchezo wa Ligi ya Mataifa ya Ulaya dhidi ya Sweden leo Jumatano.

Shirikisho la Soka nchini Ureno (PFF) limetoa taarifa kwamba kwa sasa nyota huyo wa Klabu ya Juventus anaendelea vizuri na ametengwa peke yake.

Wachezaji wengine wamepata majibu hasi baada ya kupimwa Jana Jumanne.

Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Taarifa hizi zimekuja wakati mshindi huyo mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or akiwa ameshacheza mchezo dhidi ya Ufaransa katika michuano ya Nations League na mechi ya kirafiki na Hispania.

Kabla ya taarifa hizo za Corona kutolewa, Ronaldo alishakuwa pamoja na baadhi ya wachezaji wengine kwa kusalimiana na hata kupata picha ya pamoja.

Jana Jumatatu CR7 alipost picha akiwa na wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Ureno wakiwa wanapata chakula cha pamoja.

Click to comment
 
Blog Meets Brand