-->

Type something and hit enter

On
 BAADA ya Klabu ya Manchester United kupokekea kichapo cha mabao 6-1 mbele ya Tottenham kwenye mchezo wa Ligi Kuu England inaelezwa kuwa Mauricio Pochettino amefanya mawasiliano na viongozi wa  timu hiyo ili kuweza kumpa dili.

Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Ripoti zinaeleza kuwa kichapo cha mabao 6-1 ambacho walikipokea Oktoba 4 wakiwa kwenye Uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford kimewafanya mabosi wawe na mashaka na uwezo wa Ole Gunnar Solskjaer katika kuwafikisha kwenye malengo yao waliyojiwekea.

Pochettino kwa sasa hana timu baada ya kufukuzwa ndani ya Klabu ya Tottenham ambayo alikuwa akiinoa msimu uliopita na nafasi yake kuchukuliwa na Kocha Mkuu, Jose Mourinho ambaye yupo na timu mpaka sasa.

Ndani ya miezi mitano aliyokuwa akikinoa kikosi cha Totenham, aliweza kuifikisha kwenye hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na alipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 mbele ya Liverpool mwaka 2019.

Alifukuzwa miezi 11 iliyopita kwa mpaka sasa hana timu akiwa na imani kwamba anaweza kupata timu ya kufundisha kutokana na uwezo wake wa kufundisha na aliweza kutengeneza sera nzuri na inayoeleweka katika ufundishaji huku mshambuliaji wake namba moja akiwa ni Harry Kane, nahodha Hugo LIoris na beki Toby Alderweireld.

Click to comment
 
Blog Meets Brand