-->

Type something and hit enter

On 


NYOTA watatu wa kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze huenda wakaukosa mchezo dhidi ya Biashara United unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 31.


Yanga ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Biashara United inayonolewa na Francis Baraza Uwanja wa Karume baada ya kumalizana na KMC kwa kuichapa mabao 2-1.


Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Wachezaji hao ni pamoja na Carlos Carlinhos ambaye anatibu jeraha lake la enka, Mapinduzi Balama pamoja Haruna Niyonzima ambaye anasumbuliwa na Malaria.


Kwa sasa timu ipo kambini ikiendelea na maandalizi ya mwisho ya mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.


Kwa mujibu wa Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwakila kitu kinakwenda sawa na wanatarajia kupata ushindi kwenye mchezo huo ambao utakuwa na ushinani mkubwa.


Yanga ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi zake 19 inakutana na Biashara United iliyo nafasi ya tatu kibindoni na pointi zake ni 16.

Click to comment
 
Blog Meets Brand