-->

Type something and hit enter

On
 KHALID Adam, Kocha Mkuu wa Mwadui FC amesema kuwa baada ya wachezaji wake kupokea zigo la mabao 6-1 mbele ya JKT Tanzania wakiwa nyumbani wamejipanga kuibukia mbele ya Simba, Oktoba 31, Uwanja wa Uhuru.

Mwadui FC yenye pointi tisa ikiwa nafasi ya 14 imecheza mechi 8 inakutana na Simba ambayo imecheza jumla ya mechi saba na ina pointi 13 ikiwa nafasi ya nne.


Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Zote mbili zinakutana uwanjani zikiwa zimetoka kupewa adhabu na timu za majeshi ambapo Simba wao walitunguliwa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru.

 Adam amesema kuwa alikaa na wachezaji na kuzungumza nao kuhusu suala la kupoteza na ugumu wa mchezo wao unaofuata dhidi ya Simba.

“Tumepoteza kwa kufungwa mabao mengi hilo lipo wazi, niliwaambia wachezaji kwamba makosa  yaliyopita ni lazima tusahau kisha tupambane kwa ajili ya mechi zijazo ikiwa ni pamoja na unaofuata dhidi ya Simba.

“Tunatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu hasa ukizingatia kwamba wametoka nao pia kujeruhiwa lazima watapambana kutafuta tabasamu kwetu nasi lazima tukapambane kupata pointi tatu,” amesema Adam.


Mwadui chini ya mikono ya kipa namba moja Mussa Mbissa inaongoza kwa kufungwa mabao mengi ambayo ni 14 ndani ya ligi na ni kipa wa kwanza kuokota hat trick kwa msimu wa 2020/21.


Ilikuwa mbele ya JKT Tanzania wakati Mwadui ikichapwa mabao 6-1, Uwanja wa Mwadui Complex.

Click to comment
 
Blog Meets Brand