-->

Type something and hit enter

On
 BIGIRIMANA Blaise, mtupiaji namba moja ndani ya Klabu ya Namungo FC amesema kuwa sababu kubwa inayofanya timu yao kuyumba kwa sasa ni kutokana na uwepo wa maingizo mapya ndani ya timu hiyo jambo linalowapa tabu kupata matokeo.


Kwa sasa Namungo FC ikiwa imecheza jumla ya mechi 8 ipo nafasi ya 11 na pointi zake kibindoni ni 10, imeshinda mechi tatu, sare moja na kipigo mechi nne.


Blaise ametupia mabao matatu wakati timu yake ikiwa imefunga jumla ya mabao manne ndani ya msimu wa 2020/21 ikiwa chini ya Hitimana Thiery.


Nyota huyo ambaye anakipiga pia timu ya Taifa ya Burundi amesema:"Kwa sasa tupo kwenye kipindi cha mpito ukizingatia kwamba wachezaji wengi ni wapya ndani ya kikosi bado kuna wakati unakuja tutafanya vizuri na maisha yatarejea kama ilivyokuwa zamani.


"Mashabiki watupe sapoti bado tuna nafasi ya kufanya vizuri na kwa sasa ligi bado ni mbichi, tutafanya vizuri kwenye mechi zetu zijazo," amesema.

Mchezo wao ujao ni dhidi ya Dodoma Jiji utakaochezwa Oktoba 31, Uwanja wa Majaliwa.

Click to comment
 
Blog Meets Brand