-->

Type something and hit enter

On
 UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa utapambana kupata matokeo chanya kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Uwanja wa Kaitaba.

Mtibwa inayonolewa na Vincent Barnaba ikiwa imetoka kushinda bao 1-0 dhidi ya Azam FC inakutana na Kagera Sugar iliyotoka kupoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City City.


Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar amesema kuwa kikosi kipo tayari kwa ajili ya kupambana na timu yoyote ndani ya uwanja na wana amini watafanya vizuri tofauti na msimu uliopita.


"Tulikuwa na msimu mbovu msimu uliopita ila kwa sasa tumeanza kurejea kwenye ule ubora wetu na tunafanya vizuri kwani mambo yanaonekana.


"Wale Azam FC walikuwa wanarekodi ya kutofungwa, walizifunga timu nyingi ambazo zilikuwa ndogondogo walipofika kwetu tuliwatuliza na sasa tunaendelea kupambana kwa ajili ya timu nyingine ambazo tutakutana nazo ndani ya uwanja," amesema.

Kagera Sugar haijawa na mwendo mzuri ndani ya Kaitaba kwa kuwa ilifungwa pia ilipokutana na Yanga bao 1-0 ilipokutana na JKT Tanzania pia ilifungwa bao 1-0.


Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara unatarajiwa kuchezwa Novemba Mosi. Leo Oktoba 30 tayari kikosi cha Mtibwa Sugar kimeanza safari kuifuata Kagera Sugar .

Click to comment
 
Blog Meets Brand