MRITHI WA KOCHA YANGA HUYU HAPA - EDUSPORTSTZ

Latest


 

MRITHI WA KOCHA YANGA HUYU HAPA


 Juzi, Oktoba 3, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Zlatko Krmpotic alifungashiwa virago vyake ndani ya kikosi cha Yanga baada ya kukiongoza kikosi hicho kwenye mechi 8 za ushindani.

Kocha huyo alikiongoza kikosi cha Yanga kwenye mechi tano za Ligi Kuu Bara na aliongoza kikosi hicho kwenye mechi tatu za kirafiki na kwenye mechi za kirafiki zote alishinda kwa mabao mawili mawili.


Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Aliwasili nchini Agosti 29 na kuanza kazi kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Aigle Noir ya Burundi na alishinda kwa mabao 2-0.


Kwa sasa kikosi cha Yanga kilichotoka kushinda kwa mabao 3-0 mbele ya Coastal Union kipo chini ya Kocha Msaidizi Juma Mwambusi ambaye amepewa jukumu ya kukinoa kikosi hicho kinachojiandaa na mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.


Habari zinaeleza kuwa miongoni mwa majina yaliyopo mikononi mwa Yanga ni pamoja na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Kaizer Chiefs, Ernst Middendorp ili abebe mikoba ya Krmpotic.


Ernst ni raia wa Ujerumani kwa sasa yupo Afrika Kusini akimalizia masuala ya kukabidhi ofisi kwa waajiri wake waliomfuta kazi.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz