-->

Type something and hit enter

On
 KOCHA wa Tottenham, Jose Mourinho amesema kuwa aliwatuma mabeki wake, Serge Aurier na Sergio Reguilon kuhakikisha wanadili na Marcus Rashford na Mason Greenwood, ndiyo maana wakafanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 6-1.

Wikiendi iliyopita, Spurs ikiwa ugenini kwenye Uwanja wa Old Trafford, iliibuka na ushindi huo wa mabao 6-1 dhidi ya Man United.


Mourinho alisema, aliwaelekeza mabeki wake hao nini cha kufanya huku akiwa amewalenga Rashford na Greenwood alioamini ndiyo hatari ndani ya Man United.


“Niliwaambia wachezaji wangu zaidi ya mara 1000 kuwa wanatakiwa kushinda pale Old Trafford. Na niliwapa maelekezo mabeki wangu nini cha kufanya na wadili na nani.


“Aurier na Reguilon wakishirikiana na wenzao niliwaeleza wadili zaidi na Rashford na Greenwood na hilo walifanikiwa," amesema.

Click to comment
 
Blog Meets Brand