-->

Type something and hit enter

On
 KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Luis Miquissone, raia wa Msumbiji amefunguka kwamba ataendelea na kazi ya kutengeneza mabao kwa wenzake ili kuifanya timu hiyo iendelee kupata pointi tatu kwenye mechi zake.

 

Miquissone ameongeza kwamba licha ya kutoa assisti hizo kwa wenzake lakini pia atafunga kwa sababu ni wajibu wake kikosini hapo.


Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

 

Miquissone kwenye Ligi Kuu Bara kwa msimu huu amehusika katika mabao sita ya Simba akitoa assisti tano na kufunga bao moja dhidi ya JKT Tanzania.


Miquissone raia wa Msumbiji amesema kwamba atahakikisha anaifanya kazi hiyo ya kutoa pasi za kufunga kwa wenzake kwa sababu ni sehemu ya majukumu yake ndani ya kikosi hicho kinachofundishwa na Mbelgiji Sven Vanden broeck.

 

“Najisikia vizuri kufunga na kutoa assisti kwa wenzangu kwa sababu ni sehemu ya kazi yangu, najua nina uwezo wa kupafomu vizuri.“Nafanya kazi kuisaidia timu yangu iende juu zaidi ya hapa. Nimefunga mabao mazuri na kutoa assisti lakini nataka kufunga zaidi,” aliweka

Click to comment
 
Blog Meets Brand