Mbelgiji Simba Awaweka Mtegoni Mastaa Hawa!-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mbelgiji Simba Awaweka Mtegoni Mastaa Hawa!-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amefichua kuwa tatizo kubwa la safu yake ya ushambuliaji ni kushindwa kumalizia nafasi wanazozipata ndani ya uwanja wakiwa wanapambana.

 

Raia huyo wa Ubelgiji amesema kuwa, kwenye mchezo dhidi ya Biashara United ambapo aliwatumia washambuliaji wake Chris Mugalu na Meddie Kagere wakati wakishinda mabao 4-0 tatizo lilikuwa kwenye umaliziaji.

 

“Nimegundua tatizo moja kubwa ambalo linaitesa safu yangu ya ushambuliaji ni kwenye umaliziaji wa nafasi ambazo zinatengenezwa ndani ya uwanja. Kwa kugundua tatizo hilo ninalifanyia kazi na ninaamini kwenye mechi zetu zijazo halitakuwepo,” alisema Sven.

 

Safu ya ushambuliaji ya Simba inaongozwa na vichwa vinne ambavyo ni Chris Mugalu, Meddie Kagere, Charles Ilanfya na John Bocco ambapo washambuliaji wake watatu wametupia bao mojamoja ndani ya ligi isipokuwa Ilanfya ambaye hajapata nafasi ya kucheza kwenye mechi zote tatu.

 

The post Mbelgiji Simba Awaweka Mtegoni Mastaa Hawa! appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz