-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

WAKATI mashabiki wa Yanga wakimsubiria kwa hamu kubwa kocha mpya wa timu hiyo, Cedric Kaze raia wa Burundi, imebainika kuwa kocha huyo ndiye aliyehusika na usajili wa nyota wa kikosi hicho waliosajiliwa hivi karibuni katika dirisha lililofungwa Agosti 31, mwaka huu.

 

Yanga ipo katika hatua za mwisho za kumtambulisha Kaze kuwa kocha mkuu wa kikosi hicho baada ya kuachana na Zlatko Krmpotic raia wSerbia.

Cedric Kaze raia wa Burundi.

Ikumbukwe kuwa, kabla ya Zlatko hajapewa nafasi ya kuinoa Yanga, uongozi wa timu hiyo ulifanya mazungumzo na Kaze ambaye dakika za mwisho akapata udhuru, akashindwa kujiunga na timu hiyo.

 

Wakati mazungumzo hayo yakiendelea, Kaze akahusika kufanya usajili wa nyota wa kikosi hicho akiwemo Tonombe Mukoko, Tuisila Kisinda, Songne Yacouba, Michael Sarpong, huku akihusika pia kumleta kocha wa makipa, Vladimir Niyonkuru raia wa Burundi.

 

Taarifa ambazo Spoti Xtra imezipata kutoka ndani ya Yanga zinasema kuwa, Kaze anatua Yanga akiwa kamili kwa kuwa kikosi kilichopo anahusika nacho kwa asilimia zote kutokana na kusajili baadhi ya nyota wa kimataifa, hivyo ataweza kuwatumia tofauti na ilivyokuwa kwa Zlatko.

 

“Uongozi unaendelea na mazungumzo ya mwisho na kocha Kaze ambaye atatua wakati wowote kuanzia sasa baada ya kumaliza matatizo yake ya kifamilia na kila mmoja ana matumaini makubwa na kocha huyu kwa kuwa ni mtu wa kazi, hivyo atakuja kuipa ubingwa Yanga.

“Kaze anatua Yanga akiwa kajiandaa kwani asilimia kubwa ya wachezaji waliosajiliwa msimu huu yeye anahusika kwa kiasi kikubwa kwani nyota kama Kisinda, Mukoko, Yacouba na Sarpong wote amewasajili yeye pamoja na kocha wa makipa ambaye ni chaguo lake.

 

“Amekuwa akiwasiliana mara kwa mara na kikosi, hivyo ni kocha ambaye anakijua vyema kikosi cha Yanga kuliko kocha aliyeondoka ambaye alikuwa hakijui vizuri kikosi.

“Watu wanatakiwa kuelewa kwamba, Zlatko kilichomuondoa zaidi ni kushindwa kuwatumia vizuri wale wachezaji ambao kwa kiasi kikubwa hakuhusika kwenye usajili, lakini huyu Kaze atafanya vizuri,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, alipoulizwa juu ya ujio wa kocha huyo alisema: “Wakati wowote kuanzia sasa kocha atatua na kuanza kazi mara moja.”

KHADIJA MNGWAI, DAR ES SALAAM

SHIGONGO Aomba KURA Kwa LUGHA ya KISUKUMA, WANANCHI WAMSHANGILIA

The post Mapya Yaibuka Kikosini Cha Yanga appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand