-->

Type something and hit enter

On
 USIKU wa kuamkia leo Manchester United imeibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya RB Leipzig kwenye mchezo wa UEFA hatua ya makundi.


Manchester United iliyo kundi H imecheza mchezo wake wa pili na kuibuka na ushindi huo mnono Uwanja wa Old Trafford. 


Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Kwa ushindi huo wanakuwa ni vinara wa kundi H baada ya kucheza mechi mbili na kushinda zote hivyo kibindoni wana pointi sita huku RB Leipzig ikiwa nafasi ya 3 na pointi zake ni tatu kwa kuwa imeshinda mchezo mmoja.

Shujaa wa mchezo huo alikuwa ni Marcus Rashford ambaye alitupia mabao matatu na kusepa na mpira wake jumlajumla. Alipachika mabao hayo dakika ya 74,78 na 90+2.

Mengine yalipachikwa na Mason Greenwood dakika ya 21 na Anthony Martial dakika ya 87 kwa mkwaju wa penalti.


Rashford mwenye miaka 22 aliweza kutupia pia kwenye mchezo wao uliopita wakati wakishinda dhidi ya PSG jambo linaloonesha kuwa anazidi kuwa imara.


Ole Gunnar Solksajer Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa vijana wake wanapambana na walifanya kazi kwa juhudi kusaka ushindi kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani.

Click to comment
 
Blog Meets Brand