-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KIVUMBI cha Uefa Champions League kimeendelea jana usiku na kushuhudia timu vigogo za Manchester United, Barcelona PSG na Chelsea zikiibuka na ushindi na kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa raundi inayofuata.

 

United walikuwa nyumbani Old Trafford kuikaribisha RB Leipzig ya Ujerumani na kupata ushindi mnono wa magoli 5-0, huku Marcus Rashford akiondoka na mpira baada ya kuweka kambani magoli matatu dakika ya 74, 78 90+2 akiingia kutokea benchi.  Magoli mengine yalifungwa na kinda Mason Greenwood dakika ya 21 na Athony Martial dakika ya 87 aliyefunga kwa mkwaju wa penati.

 

Kwa matokeo hayo Manchester United wanaongoza kundi H kwa pointi sita wakifuatiwa na PSG amba0 walishinda jana dhidi ya Instanbul Basaksehir ya Uturuki kwa mabao 2-0.

 

Mechi nyingine kali ilikuwa  Italia kati ya Juventus dhidi ya Barcelona, mechi iliisha kwa ushindi wa magoli 2-0 mabao yakifungwa na Osman Dembele 14, na nahodha Lionel Messi kwa mkwaju wa penati dakika ya 90.  Vibibi vizee vya Turin vilicheza bila ya staa wao Cristiano Ronaldo ambaye bado ana virusi vya Corona.

 

Chelsea wakiwa ugenini walifanikiwa kushinda magoli 4-0 dhidi ya Krasnodar ambapo  magoli ya The Blues hao yalifungwa na Callum Hudson Odoi dakika ya 37, Timo Werner dakika ya 76, Hakim Zayech dakika ya 79 na Christian Pulisic 90.

 

The post Man United Chelsea Zatakata Uefa appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand