-->

Type something and hit enter

On
 IKIWA kwa sasa Yanga ipo kwenye mchakato wa kumtafuta Kocha Mkuu atakayebeba mikoba ya Zlatko Krmpotic ambaye walifikia naye makubaliano ya kuachana naye Oktoba 3 kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kutoridhishwa na mwendo wake tayari majina yapo mezani mwa Yanga.


Habari zinaeleza kuwa kwa sasa ndani ya Yanga kuna majina mengi ambayo yanafanyiwa uchunguzi wa sifa za makocha hao huku ikiwa ni pamoja na orodha iliyopita kabla ya kumtangaza kocha huyo.

Miongoni mwa wanaotajwa kuwa kwenye hesabu za Yanga ni pamoja na George Lwandamina raia wa Zambia ambaye aliwahi kuifundisha Yanga na kuipa taji la Ligi Kuu Bara msimu wa 2016/17.

 Kaze Cedric raia wa Burundi huyu anapewa nafasi kubwa ya kuibukia ndani ya Yanga kwa kuwa mchakato wake ulisitishwa mwishoni kabla ya ligi kuanza kwa kueleza kuwa alikuwa na matatizo ya kifamilia na Ernst Middendorp raia wa Ujerumani.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa mchakato kwa sasa wa kutafuta kocha mpya unaendelea.

Click to comment
 
Blog Meets Brand