-->

Type something and hit enter

On
 ROMELU Lukaku nyota wa kikosi cha Inter Milan amesema kuwa anaamini kwamba yupo huru kwenye kutupia mabao mengi akiwa ndani ya Italia kuliko alipokuwa England.

Lukaku aliibukia ndani ya Inter Milan akitokea Klabu ya Manchester United kwa dau la Euro milioni 73.


Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Akiwa ndani ya Milan raia huyo wa Ubelgiji ametupia jumla ya mabao 37 kwenye mechi 53 ambazo amecheza kuanzia msimu wa 2019 akiwa San Siro.

Alitimiza majukumu yake kwa kuifikisha timu yake kwenye fainali ya Europa League alifunga bao moja mapema kabisa kabla ya kujifunga bao lililoipa ushindi Sevilla wakati wakipoteza kwa kufungwa mabao 3-2.

Lukaku ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu ndani ya Europa League msimu huu baada ya kufunga jumla ya mabao saba.

Nyota huyo amesema :"Mwaka mmoja uliopita wakati nilipokuwa  England, wengi walikuwa wakiniona mimi ni mjinga, siwezi kufanya jambo lolote, mvivu, siwezi kukimbia siwezi kufanya jambo jingine yaani siwezi kufanya hivi na vile.

'Hapa nilipo kwa sasa wananiita mpambanaji, ninafanya kazi kweli hasa tukiwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, hata ukiniangalia mimi namna ninavyocheza ninaona mabadiliko makubwa, unaona yale ambayo nilipaswa kuyafanya nikiwa England unamuona mtu mwenyewe anayefanya kazi kwa nguvu."

Click to comment
 
Blog Meets Brand