-->

Type something and hit enter

On
 KIUNGO mshambuliaji wa Simba raia wa Msumbiji Luis Miqquisone, ametengeneza rekodi ya kwanza kuwa mchezaji anayeongoza kwa kuwa na kadi nyingi za njano katika kikosi hicho.

 

Nyota huyo hivi karibuni aliweka rekodi ya kupiga asisti tatu katika mchezo mmoja wa Ligi Kuu Bara walipocheza dhidi ya Biashara United, uliomalizika kwa timu hiyo kufunga mabao manne.


Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

 

Katika mchezo huo aliwatengenezea mabao Mzambia, Clatous Chama, aliyempa pasi mbili za mabao kabla ya kumtengea Mnyarwanda, Meddie Kagere. Staa huyo baada ya rekodi ya asisti ya mabao, akaja na hiyo ya kuongoza na kadi mbili za njano akicheza michezo mitatu ya ligi tangu kuanza kwa msimu huu.

 

Michezo hiyo aliyopata kadi ni dhidi ya Biashara United uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam na ule dhidi ya JKT Tanzania uliochezewa Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

 

Aidha, nyota huyo hadi hivi sasa amefanikiwa kufunga bao moja pekee tangu kuanza kwa msimu huu katika ambalo alilifunga kwenye mchezo dhidi ya JKT.

 

Luis anatakiwa kucheza kwa nidhamu kubwa ili asipate kadi nyingine ya tatu itakayomsababishia aukose michezo inayofuatia ukiwemo dhidi ya Yanga, kwa mujibu wa kanuni za soka zinamtaka mchezaji kukosa mchezo mmoja unaofuatia akiwa na kadi tatu za njano.

Click to comment
 
Blog Meets Brand