-->

Type something and hit enter

On
 LIGI ya Mabingwa Barani Afrika imeendelea mwishoni mwa wiki hii,  ikiwa ni hatua ya nusu fainali kwa miamba ya soka  Afrika ya Kaskazini Morocco na Misri kutoana jasho vilivyo, ambapo National Al Ahly  wakiwa chini ya kocha mpya Pitso Mosimane walikuwa ugenini kuvaana na Wydad Casablanca ya Morocco.

Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Kwenye mchezo huo Al Ahly iliweza  kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kujiweka katika mazingira mazuri katika mechi ya marudiano itakayochezwa Misri.

 

Pitso Mosimane ambaye ajiuzulu kuifundisha Mamelodi Sundowns ya Afrika ya Kusini mara baada ya kutwaa ubingwa,  ameonyesha ni kwa  jinsi gani anaweza kuipa taji  Al Ahly la Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi huo wa ugenini wakisubiri kumaliza kazi nchini Misri.

 

Timu hiyo ambayo inaongoza kwa utajiri Afrika ilifunga magoli yake kupitia kwa Mohamed Magdy dakika ya nne na bao la pili likiwekwa kimiani na Ali Maaloul kwa mkwaji wa penati dakika ya 62.


Nusu fainali nyingine iliwashuhudia Raja Casablanca  wakiwakaribisha vigogo wengine,  Zamelek wa Misri ambapo walikubali kipigo cha bao 1-0  bao pekee la Zamelek likifugwa na Achraf Bencharki dakika 18 ambapo mechi za marudiano zitachezwa  tarehe 23 mwezi huu.

 

 Huenda ikashuhudiwa fainali  kati ya  timu za Misri ila ni jambo la kusubiri baada ya wiki moja majibu yatapatikana.

Click to comment
 
Blog Meets Brand