-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KINARA wa pasi za mwisho kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu na nyota wa klabu ya Simba, Luis Miquissone ‘Konde Boy’ amesema kuwa achana na alichokifanya kwenye michezo mitano iliyopita kwani amejipanga kuuwasha moto mkali zaidi pale ligi itakaporejea baada ya mapumziko ya kupisha michezo ya kimataifa.

 

Luis amekuwa moto wa kuotea mbali msimu huu ambapo amehusika kwenye mabao sita kati ya 14 ambayo Simba imefunga kwenye michezo yao mitano iliyopita.

 

Akizungumzia kiwango chake Luis alisema: “Namshukuru Mungu kwa kuwa na mwanzo mzuri msimu huu, ambapo kwenye michezo mitano iliyopita nimefanikiwa kufunga bao moja na kuasisti mara tano, kwangu nimekuwa nikisema mara zote kuwa natamani kufanya vizuri kwenye kila mchezo kwa ajili ya mafanikio ya Simba.

 

“Kiwango nilichofanikiwa kukionyesha kwenye michezo iliyopita na ushindani wa namba uliopo kwenye kikosi vimezidi kunipa ari ya kutaka kufanya vizuri zaidi, hivyo naamini nitakuwa moto zaidi kwenye michezo ijayo baada ya mapumziko ya kupisha michezo ya kimataifa kumalizika,” alisema kiungo huyo raia wa Msumbiji.

Joel Thomas, Dar es Salaam

The post Konde Boy Atangaza Hali ya Hatari appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand