-->

Type something and hit enter

On
 KOCHA mkuu wa Klabu ya Indeni ya Zambia, David Chilufya, amesema haikuwa bahati mbaya kwake kumpa mkataba wa miaka miwili aliyekuwa beki wa Yanga, Juma Abdul kwa kuwa anajua ubora wake ndani ya uwanja.

 Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Beki huyo amejiunga na timu hiyo yenye makazi yake katika mji wa Ndola ambayo imepanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Zambia, msimu huu unaotarajia kuanza mwezi ujao.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Chilufya alisema kuwa hakumsajili beki huyo kwa bahati mbaya kwa kuwa anaujua vizuri uwezo wake baada ya kumuona wakati Yanga ilipocheza na Zesco katika Kombe la Shirikisho Afrika.“Ni kweli Juma amejiunga na timu yetu kwa mkataba wa miaka miwili, nilimuona mwenyewe nilipokuja Tanzania wakati nilipokuwa na Zesco kucheza na Yanga hivyo namjua vizuri wala sina shida naye.

 

“Kiukweli nina imani kubwa juu yake katika nafasi ambayo anacheza lakini naamini atakuwa msaada kwa kuwa yeye ni mchezaji mwenye uzoefu kwa sababu timu yetu bado ni changa kwenye ligi ya hapa,” alisema Chilufya.

Click to comment
 
Blog Meets Brand