-->

Type something and hit enter

On
 CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wachezaji wake wote wanajituma ndani ya Uwanja ikiwa ni pamoja na Farid Mussa ambaye ameanza kuwa bora Kwenye mechi mbili za hivi karibuni.


Yanga ikiwa imefunga mabao 10 amehusika Kwenye mabao mawili ambapo alitoa pasi ya Kwanza Uwanja wa Uhuru wakati Yanga ikishinda bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania na alitoa pasi yake ya pili dhidi ya KMC wakati Yanga ikishinda mabao 2-1, Uwanja wa CCM Kirumba. 


Yanga inakutana na Biashara United Oktoba 31 Uwanja wa Karume ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 19 inakutana na Biashara United iliyo nafasi ya tatu Kwenye msimamo.


Kaze amesema:-"Wachezaji wanajituma na wanafanya kazi ya kusaka ushindi, kwa sasa ninaona kwamba kila mmoja anauwezo mkubwa na ninapenda kuona kuwa wanaendelea kuwa bora ikiwa ni pamoja na Farid Mussa,  Wazir Junior kila mchezaji ana umuhimu ndani ya kikosi."

Click to comment
 
Blog Meets Brand