-->

Type something and hit enter

OnKOCHA SIMBA ATAJA MATATIZO MAWILI YANAYOKITESA KIKOSI HICHO


 JAMHURI Khwelo aliyewahi kuwa kocha wa timu hiyo amesema kuwa kikosi cha Simba kina matatizo makubwa mawili ambayo yanakisumbua kwa sasa jambo ambalo linawafanya wapate matokeo mabovu ndani ya uwanja.


Mabingwa hao watetezi wamekutana na vipigo viwili mfululizo na kuziacha alama sita zikisepa na upepo ndani ya Ligi Kuu Bara.

Walipoteza mbele ya Tanzania Prisons kwa kufungwa bao 1-0 wakiwa ugenini kwenye Uwanja wa Nelson Mandela kisha wakiwa nyumbani walitembezewa kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Uhuru.

Leo Oktoba 31 Simba ina kibarua cha kusaka pointi tatu muhimu mbele ya Mwadui FC Uwanja wa Uhuru.

Julio amesema:"Kwa sasa Simba wanapambana na matokeo magumu kutokana na mambo mawili ambayo wanayo kwanza ni umri wa wachezaji wengi kuwatupa mkono jambo linalowafanya wapate tabu kuhimili mikikimiki ndani ya uwanja.

"Pili ni suala la majeruhi wengi ambao wapo kwa Simba kwa sasa, jambo hilo linafanya kocha awe kwenye wakati mgumu kutafuta matokeo na kuwa na kikosi kitakachoipa ushindi ndani ya uwanja.

"Wachezaji wakipata majeraha inachukua muda mrefu kupona na inapotokea ishu ya kubadilisha kikosi wengi wanashangaa na matokeo yanapokuja tofauti inakuwa ni makelele kwa mashabiki kwa kuwa hawajazoea kuona mambo hayo," amesema.

Click to comment
 
Blog Meets Brand