-->

Type something and hit enter

On
 FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Biashara United amesema kuwa amewaambia wachezaji wake wapambane na kila mchezaji atakayekuwa na jezi ya njano uwanjani bila kujali uwezo wake upoje ndani ya uwanja.


Kesho, Oktoba 31 Biashara United iliyo nafasi ya tatu kwenye msimamo na pointi 16 itamenyana na Yanga iliyo nafasi ya pili ikiwa na pointi 19.


Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Akizungumza na Saleh Jembe, Baraza amesema kuwa maandalizi ya kikosi yapo vizuri na wanaamini kwamba watapata matokeo kwenye mchezo wa kesho.


"Nimewaambia wachezaji kwamba wana jukumu la kuambana na kila mchezaji mwenye jezi ya njano ndani ya uwanja bila kujali uwezo wa wapinzani wangu.


"Ni wacheche kwa sasa ambao wamefungwa mabao machache ndani ya ligi ambao ni Yanga sasa kazi kubwa itakuwa kwenye kusaka ushindi hilo lipo wazi lakini tutapambana," amesema.


Safu ya ulinzi ya Yanga imeruhusu mabao mawili ya kufungwa ndani ya ligi ikiwa imecheza jumla ya mechi saba huku ile ya Biashara United ikiwa imeruhusu kufungwa mabao saba baada ya kucheza mechi nane.

Click to comment
 
Blog Meets Brand