-->

Type something and hit enter

On
 Baada ya kupoteza mchezo wa mzunguuko watano dhidi ya Polisi Tanzania FC, Kikosi cha KMC FC Leo Jumatano Oktoba 14 kitaendelea na Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union kutoka jijini Tanga.

Mchezo huo wa mzunguuko wasita utachezwa Uwanja wa Uhuru, kuanzia mishale ya saa kumi jioni, huku ukitarajiwa kuwa na upinzani wa vuta nikuvute kwa kuwa timu zote zimetoka kupoteza alama tatu kwenye michezo iliyopita.

Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Coastal Union walipoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Young Africans kwa kufungwa mabao matatu kwa sifuri, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam.

Ofisa Habari wa KMC Christina Mwagala, amesema kuwa makosa waliyoyafanya kwenye michezo miwili iliyopita, wameyaona na wameshafantiw kzi n benchi la ufundi linaloongozwana kocha mzawa Habibu Kondo.

 “Tulipoteza mchezo wetu wa kwanza uwanja wa nyumbani haina maana kwamba tutaendelea kupoteza hapana bado tuna mechi nyingi na tutaanza na Coastal Union Uwanja wa Uhuru Jumatano tunaamini tutafanya kweli.

“Mashabiki wasikate tamaa mapambano bado yanaendelea na KMC ina wachezahi wazuri wenye uwezo hivyo kwa sasa ni wakati wa kuendelea kupeana sapoti ili kupata matokeo chanya,” amesema.

KMC ipo nafasi ya saba ikiwa imecheza michezo mitano ina alma 9 kibindoni, inakutana na Coastal Union ambayo imecheza michezo mitano na ina alama nne ikiwa nafasi ya 15.

Click to comment
 
Blog Meets Brand